Watanzania wakipata msaada muafaka watainua kilimo, asema Kirenga

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bwana George Simbachawene   (kulia) akibadilishana mawazo na  Mkuu wa Kongani katika shirika la Sagcot Bibi Maria Ijumba (kushoto karibu na kamera),katikati ni Afisa Mtendaji wa Sagcot, Bw. Geoffrey Kirenga Jijini Mbeya wakati wa kabla ya kufunga maonyesho ya Nane Nane leo (Picha na Moses Ferdinand).

Na Rukiza Kyaruzi, Jijini Mbeya

Wakati serekali  na wadau maarufu wanafanya  jitihada kubwa kuirudishia mikao ya nyanda za juu kusini heshima yake ya kuwa ‘kapu la chakula la taifa’  maonyesho ya shughuli za kilimo, maarufu kama NaneNane  yaliyofanyika Jijini Mbeya hivi karibuni ( Agosti 8, 2017) Sagcot  imeyaona maonyesho hayo kuwa  ni fursa waliyotumia  Watanzania  kuonyesha uwezo wao katika kilimo  na kupokea changamoto mpya.

Akitoa salaamu za Kituo cha Kuendeleza Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT),  Mkurugenzi Mtendaji , Bwana Geoffrey Kirenga, ameeleza hadhara ya ufungaji wa maonyesho hayo kwamba maonyesho hayo yamedhahirisha uwezo wa Watanzania katika kuinua kilimo ili kiwe uti wa mgongo wa kweli  wa Tanzania ya uchumi wa kati ambao utategemea viwanda.

Mkurugenzi Mtendaji huyo ameeleza kuwa  Watanzania wakipewa msaada wakati unaofaa wataleta mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo.

“Watanzania”, aliuhakikisha umma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bwana George Simbachawene , “wako tayari kupokea utaalamu katika kilimo… Wakipewa msaada wakati unaofaa wateleta mbadiliko makubwa.”

Waziri Simbachawene alimuwakilisha Makamu wa Rais, Bi Samia Saluhu Hassani,  kufunga maonyesho hayo.

Maonyesho ya Mbeya yaliilenga mikoa ya nyanda za juu kusini na ilikuwa ni furusa ya wadau wote wakilimo kuonyesha  mafanikio, changamoto, matatizo na fursa zilizomo katika kilimo.

Bw. Kirenga ameomba  vyombo vinavyohudumia kilimo viungwe mkono  haraka iwezekanavyo  kila vinapohiji msaada. “Taasisi au mashirika yanayojihusisha na kilimo yanahitaji kupata huduma za haraka na zenye ufanisi ili kuleta tija katika kilimo,” ameeleza Bw. Kirenga.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amerudia kueleza  kuwa Tanzania ya viwanda itawezekana na kustawi tu iwapo ufanisi utakuwa katika kila  shughuli inayofanywa.  Ameeleza kuwa shughuli zinazohusu kuimarisha kilimo na kumuhudumia mkulima lazima zibebe ndani yake ufanisi. “Tunapokwenda katika Tanzania ya viwanda lazima huduma hizi zitolewe kwa ufanisi zaidi,” alisema Bw. Kirenga.

Mapema akihutubia hadhara hiyo Waziri Simbachawene amewaomba wakulima katika mikoa ya nyanda za juu kusini   kulipa umuhimu mkubwa suala la kutumia sayansi na tekinolojia ili kurejesha sifa ya mikoa hiyo  kuwa ‘kapu la chakula la taifa’ .

Waziri amesema kaulimbiu ya mwaka huu inatoa ujumbe mahususi juu ya umuhimu wa kuzalisha mazao bora ya kilimo ambayo yanaingiza zaidi ya asilimia 65 ya malighafi za viwandani, lakini akaongeza bado mkulima anavuna kiasi kidogo cha mazao katika hekta moja.

Ametoa mifano kadhaa kuonyesha kwamba mkulima hanufaiki na jasho lake katika kila hekta anayolima na kupanda mazao au kutokana na ufugaji.

Akitoa mfano wa zao la mahindi waziri amesema  kwa sasa katika hekta moja mkulima wa mdogo wa Tanzania tani 3 wakati utafiti unaonyesha kuwa anastahili kupata tani saba na zaidi za mahindi.

Waziri amesema katika hekta moja mwanakijiji anastahili kupa tani 30 katika hekta kwa mujibu wa matokeo ya utafiti, lakini sasa anapata tan inane tu.

Bw. Simbachawene ameeleza kuwa ng’ombe mmoja anastahili kumzawadia mwanakijiji kati ya lita 20 mpaka 40 za maziwa kwa siku, lakini sana mkulima anapata lita 8 tu.

Mazao yote ambayo ameyotolea mfano waziri yanalimwa katika mikoa ya nyanda za juu kusini.

Pichani juu:

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bwana George Simbachawene   (kulia) akibadilishana mawazo na  Mkuu wa Kongani katika shirika la Sagcot Bibi Maria Ijumba (kushoto karibu na kamera),katikati ni Afisa Mtendaji wa Sagcot, Bw. Geoffrey Kirenga Jijini Mbeya wakati wa kabla ya kufunga maonyesho ya Nane Nane leo (Picha na Moses Ferdinand).

Share

clement

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *