Wakulima Njombe waishukuru Sagcot kwa mafunzo ya kilimo cha viazi mviringo

Picha ya pamoja ya wadau walionufaika na mpango wa mafunzo wa miaka mitatu baada sherehe ya ufungaji wa mafunzo hayo Jijini Mbeya leo Ijuma (Septemba 15. 2017). Mafunzo hayo yalifungwa na Katibu Tawala Msaidizi (Uchumi na Sekta Uzalishaji) Mkoa wa Njombe, Bw. Lameck Noah. (Picha kwa hisani ya Prosper Mfugale)

Na Mwandishi Wetu, Njombe
TANZANIA ni miongoni mwa nchi zinazotazamiwa kunufaika na fursa nyingi za
katika uzalishaji wa  viazi mviringo kutokana na ushirikiano madhubuti
kati ya serikali na sekta binafsi katika kuinua kilimo cha wakulima wadogo.
Akizungumza katika mkutano wa kufunga mafunzo ya uzalishaji viazi
yaliyodumu  katika program ya  miaka mitatu kwa wakulima wa Njombe leo (Ijumaa, Septemba 15, 2017), Mkuu wa  Maendeleo ya Kongani kutoka Kituo cha Kuendeleza Kilimo
Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania (Sagcot), Bi. Maria Ijumba, amesema
kutokana na matokeo chanya ya mafunzo hayo haoni taifa litakaloipita
Tanzania katika kilimo hicho kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na hata
kusini mwa Jangwa la Sahara.
“Tulipoanza hatukuwa na watu wa kujitolea lakini tulitaka kuwaonyesha
wakulima namna fursa za kilimo cha viazi zilivyo; sekta binafsi
imechangamka sasa naamini hakuna wa kutufikia kwa sababu changamoto
zote tumezipatia ufumbuzi,” alisema Mama Ijumba na kuongeza:
“Serikali ya Uholanzi imeahidi kuanzisha kituo cha kuonyesha fursa za
viazi eneo la Uyole mkoani Mbeya, vilevile zipo kampuni zinazoleta
mashine za kurahisisha upandaji na uvunaji viazi. Kazi iliyobaki ni
wakulima kuonyesha elimu waliyopata imewafaa.”
Alibainisha kuwa kwa sasa zao la viazi limekua mkombozi wa wakulima
wengi katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na mikoa jirani kwa sababu
awali walikuwa wakifanya kilimo cha kimazoea lakini sasa kipato
kinaonekana kwa sababu uzalishaji umeongezeka na biashara inafanyika.
“Kwa sasa viazi kama zao la biashara limeshika kasi. Hakika hiki
tulichoanzisha kitakua endelevu na tunaamini zao hili litawakomboa
wakulima. Hadi sasa kuna vikundi zaidi ya 50 vilivyoundwa na wakulima,
ifahamike kuwa wakulima wakiwa pamoja na wakiendelea kupata elimu
watafanikiwa kwa sababu mkulima mdogo hawezi kuendelea peke yake,”
alisema Mama Ijumba.
Kwa upande wake, Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Sekta Uzalishaji
Mkoa wa Njombe, Bw. Lameck Noah aliyekuwa mgeni rasmi katika mkutano
huo alisema kazi iliyobakia kwao ni kuhakikisha mafunzo waliyopata  wakulima na wataalamu wa kilimo yanaunufaisha mkoa mzima.
“Halmashauri itaendelea kufuatilia wakulima wanaozalsiha mbegu na
wanaozalisha mazao pamoja na wataalamu wa kilimo iili waendelee kutoa
huduma ya ugani. Kwa kutumia huu ubia kati ya serikali na sekta
binafsi tutaomba fedha ili kuendeleza shughuli za kilimo,” amesema Bw.
Noah.
Amesemakizungumzia mafanikio yaliyopatikana katika mkoa wake kupitia Sagcot imefanya kazi kubwa na kwmba inaacha alama kwa
wakulima na wadau wengine wa kilimo katika kutambua fursa zilizopo.

 

Bibi Leah Nsilu kutoka Kata ya Matembwe mkoani humo amesema mafunzo ya miaka mitatu yamebadili mtazamo wao katika kilimo cha zao hilo.  Amesema  mafunzo yalianza vizuri kwa kuwaeleza wakulima namna ya kutumia mbolea na viatilifu ili kupata
mazao bora.
“Huu ni mwaka wa tatu tangu tuanze mafunzo, tumenufaika sana. Mwaka wa
kwanza tulianza mafunzo ya kutumia mbolea, tukaanza kulima bondeni na
kupanda shambani mafanikio yalikua mazuri. Tulikuwa tunaonyeshwa namna
tofauti iliyopo kati ya kilimo cha zamani tulichokuwa tukifanya
kiamzoea na kilimo cha kisasa.
“Baada ya mafunzo haya wanakikundi cha ushirikiano Matembwe, tunasema
haturudi nyuma tutaendelea na kilimo kwa sababu zamani hatukua
tukilima viazi kwa sababu hatukujua faida yake lakini sasa tunasomesha
watoto na kujenga nyumba kwa kutumia viazi,” alisema Bibi Nsilu.
Shughili za SAGCOT zinafadhiliwa na Serikali ya Tanzania, Shirika la
Misaada na Mawndeleo la Uingereza(UKAID), Ubalozi wa Norway nchini,
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Maendeleo(UNDP), Shirika la Misaada
la Marekeni (USAID), Benki ya Dumia na AGRA.

Share

clement

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *